METHALI MIA SITA NA KUMI (610)

 1. Aanguaye huanguliwa.
 2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu.
 3. Abebwaye hujikaza.
 4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti.
 5. Adui aangukapo, mnyanyue.
 6. Adui mpende.
 7. Adui wa mtu ni mtu.
 8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna.
 9. Ahadi ni deni.
 10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
 11. Akiba haiozi.
 12. Akili ni mali.
 13. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
 14. Akili nyingi huondowa maarifa.
 15. Akutukanae hakuchagulii tusi.
 16. Akipenda chongo huita kengeza.
 17. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki.
 18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema.
 19. Akupaye kisogo si mwenzio.
 20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
 21. Alisifuye jua, limeuangaza.
 22. Aliye juu msubiri chini.
 23. Aliye kando, haangukiwi na mti.
 24. Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi.
 25. Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua.
 26. Akufukuzae hakwambii toka.
 27. Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa.
 28. Amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga.
 29. Ana hasira za mkizi.
 30. Anayekuja pasi na hodi, huondoka bila ya kuaga.
 31. Angurumapo simba, mcheza ni nani?
 32. Aninyimaye mbazi kanipunguzia mashuzi.
 33. Apewaye ndiye aongezwaye.
 34. Anaejipiga mwenyewe, halii.
 35. Asifuye mvuwa imemnyea.
 36. Asiye kubali kushindwa si mshindani.
 37. Asiye kujua, hakuthamini.
 38. Asiye kuwapo na lake halipo.
 39. Asiye lelewa na mamae hulelewa na ulimwengu.
 40. Asiye na mengi, ana machache.
 41. Asiye uliza, hanalo ajifunzalo.
 42. Asiyejua maana, haambiwi maana.
 43. Atangaye na jua hujuwa.
 44. Atangazaye mirimo, si mwana wa ruwari (Liwali).
 45. Atekaye maji mtoni hatukani mamba.
 46. Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
 47. Baada ya dhiki faraja.
 48. Bahari hailindwi.
 49. Bamba na waume ni bamba, hakuna bamba la mume.
 50. Bandu bandu huisha gogo.
 51. Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
 52. Bendera hufuata upepo.
 53. Biashara asubuhi.
 54. Bilisi wa mtu ni mtu.
 55. Bora kinga kuliko tiba.
 56. Bora lawama kuliko fedheha.
 57. Bora mchawi kuliko fitina.
 58. Biashara asubuhi.
 59. Bora nusu shari kuliko shari kamili.
 60. Bwawa limeingia ruba.
 61. Cha mtu mavi.
 62. Chaka la samba, halilali nguruwe.
 63. Chamlevi huliwa na mgema.
 64. Chanda chema huvikwa pete.
 65. Chelewa chelewa, utakuta mtoto si wako.
 66. Choko mchokoe pweza, binaadamu hutomuweza.
 67. Chombo cha kuzama hakina usukani.
 68. Chovya – chovya yamaliza buyu la asali.
 69. Chui hakumbatiwi.
 70. Chururu si ndo ndo ndo.
 71. Dalili ya mvua mawingu.
 72. Damu nzito kuliko maji.
 73. Daraja livuke ulifikapo.
 74. Dawa ya moto ni moto.
 75. Daraja ukilibomoa, ujue kuogelea.
 76. Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda joshi ni matakwa ya Mungu.
 77. Dawa ya moto ni moto.
 78. Donda ndugu halina dawa.
 79. Dua ya kuku haimpati mwewe.
 80. Fadhila huna, hata hisani hukumbuki?
 81. Fadhila ya nyuki ni moto.
 82. Fadhila ya punda ni mateke (mashuz)
 83. Fahari ya macho haifilisi duka.
 84. Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
 85. Fata nyuki ule asali.
 86. Fimbo ya mbali haiui nyoka.
 87. Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua.
 88. Funika kombe mwanakharamu apite.
 89. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
 90. Gome la udi, si la mnuka uvundo.
 91. Haba na haba, hujaza kibaba.
 92. Haki ya mtu hailiki.
 93. Hakuna masika yaso mbu.
 94. Hakuna msiba usio na mwenziwe.
 95. Hakuna siri ya watu wawili.
 96. Hakuna ziada mbovu.
 97. Hala hala mti na macho.
 98. Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi.
 99. Hapana marefu yasio na mwisho.
 100. Haraka haraka haina baraka.
 101. haraka haraka haina baraka.
 102. Haramu yako halali kwa mwenzio.
 103. Hasidi hasada.
 104. Hasidi mbaya.
 105. Hasira, hasara.
 106. Hatua ndefu hufupisha mwendo.
 107. Hauchi hauchi, unakucha.
 108. Hayawi hayawi, mara huwa.
 109. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
 110. Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
 111. Heri nitakula na nini?, kuliko nitakula nini?
 112. Heri ya marama kuliko kuzama.
 113. Hiari ya shinda utumwa.
 114. Hogo halihogoki mpaka kwa hogo jenziwe.
 115. Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
 116. Ila ya kikwapa, kunuka pasipo kidonda.
 117. Yaliyoopita si ndwele, ganga yajayo.
 118. Iliyo jaa ndiyo ipunguzwayo.
 119. Imara ya jembe kaingojee shambani.
 120. Jambo usilolijua, usiku wa giza.
 121. Jina jema hungara gizani.
 122. Jini likujualo halikuli likakwisha.
 123. Jino la pembe si dawa ya pengo.
 124. Jitihada haiondoi kudura.
 125. Jitihadi haiondoi kudura.
 126. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
 127. Jungu kuu, halikosi ukoko.
 128. Jununu fununu.
 129. Kafiri akufaaye, si muislamu asiye kufaa
 130. Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
 131. Kama hujui kufa,tazama kaburi.
 132. Kama wewe wasema cha nini, mwezio asema nitakipata lini.
 133. Kamba hukatika pabovu.
 134. Kanga hazai ugenini.
 135. Kawaida ni kama sheria.
 136. Kawia ufike.
 137. Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
 138. Kelele za chura hazimzuwii ng’ombe kunywa maji.
 139. Kelele za mlango haziniwasi usingizi (Kelele za mlango hazimuudhi mwenye nyumba)
 140. Kenda karibu na kumi.
 141. Kesho kesho, kesho kiama.
 142. Kiburi si maungwana.
 143. Kibuzi na kibuzi hununua jahazi.
 144. Kichango kuchangizana.
 145. Kidole kimoja hakivunji chawa.
 146. Kikulacho ki nguoni mwako.
 147. Kikushindacho kukila usikitie ila.
 148. Kila chombo kwa wimblile.
 149. Kila mbwa hubwekea mlangoni kwao.
 150. Kila mlango na ufunguwo wake.
 151. Kila mtoto na koja lake.
 152. Kila mtu huzikwa na kaburi lake.
 153. Kila mtu na bahati yake.
 154. Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.
 155. Kila mtu hulilia mamae.
 156. Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
 157. Kila shetani na mbuyu wake.
 158. Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua.
 159. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
 160. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
 161. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
 162. Kingiacho mjini si haramu.
 163. Kinyozi hajinyoi.
 164. Kinywa ni jumba la maneno.
 165. Kipendacho moyo dawa.
 166. Kipofu hasahau mkongojo wake.
 167. Kipya kinyemi ingawa kidonda.
 168. Kisebusebu na kiroho papo.
 169. Kisokula mlimwengu, sera nale.
 170. Kisokula mlimwengu,sera nale.
 171. Kisu kimenifika mfupani.
 172. Kitanda usicho kilalia hukijui kunguni wake.
 173. Kitumbua kimeingia mchanga.
 174. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
 175. Kiwi cha yule ni chema cha; hata ulimwengu uwishe.
 176. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
 177. Konzi ya maji, haifumbatiki.
 178. Konzo ya maji haifumbatiki.
 179. Kosa moja haliachi mke.
 180. Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda.
 181. Kuagiza kufyekeza.
 182. Kuambizana kuko kusikilizana hapana.
 183. Kucha M’ngu si kilemba cheupe.
 184. Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi.
 185. Kufa kufaana.
 186. Kufa kwa jamaa, harusi.
 187. Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.
 188. Kufanaya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa.
 189. Kuishi kwingi, kuona mengi.
 190. Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.
 191. Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
 192. Kukopa harusi kulipa matanga.
 193. Kukopa harusi, kulipa matanga.
 194. Kuku havunji yai lake.
 195. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
 196. Kula kutamu ,kulima mavune.
 197. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
 198. Kukopa harusi, kulipa matanga.
 199. Kumuashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.
 200. Kunako matanga kume kufa mtu.
 201. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
 202. Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma.
 203. Kupata si werevu, na kukosa si ujinga.
 204. Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
 205. Kurambaramba ndio kula, kunenepa kwake Mola.
 206. Kusikia si kuona.
 207. Kutangulia si kufika.
 208. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
 209. Kutu kuu ni la mgeni.
 210. Kuugua sio kufa.
 211. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
 212. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
 213. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
 214. Kweli ilio chungu, si uongo ulio mtamu.
 215. Kwenda mbio siyo kufika.
 216. Kwenye miti hakuna wajenzi.
 217. La kuvunda halina rubani.
 218. La kuvunda halina ubani.
 219. Lake mtu halimtapishi bali humchefua.
 220. Leo kwako, kesho kwa mwenzio.
 221. Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
 222. Liandikwalo ndiyo liwalo.
 223. Lila na fila hazitangamani.
 224. Lipitalo, hupishwa .
 225. Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
 226. Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.
 227. Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
 228. Maafuu hapatilizwi.
 229. Macho hayana pazia.
 230. Mafahali wawili hawakai zizi moja.
 231. Maiti haulizwi sanda.
 232. Maji hayapandi mlima.
 233. Maji hufuata mkondo.
 234. Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaoga.
 235. Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
 236. Maji ya kifuu, bahari ya chungu.
 237. Maji yakijaa hupwa.
 238. Maji yakimwagika hayazoleki.
 239. Maji yamenifika shingoni.
 240. Majuto ni mjukuu.
 241. Mali ya bahili huliwa na wadudu.
 242. Mama ni mama, hata kama ni rikwama.
 243. Mama nipe radhi kuishi na watu kazi.
 244. Mambo kunga.
 245. Manahodha wengi chombo huenda mrama.
 246. Maneno makali hayavunji mfupa.
 247. Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni.
 248. Maneno si mkuki.
 249. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
 250. Masikini akipata matako hulia mbwata.
 251. Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba.
 252. Masikini na mwanawe tajiri na mali yake.
 253. Maskini hana kinyongo.
 254. Mavi usioyala, wayawingiani kuku?
 255. Mavi ya kale hayanuki.
 256. Mbinu hufuata mwendo.
 257. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
 258. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
 259. Mchagua jembe si mkulima.
 260. Mchagua nazi hupata koroma.
 261. Mchagua nazi si mfuaji.
 262. Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
 263. Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo.
 264. Mchamba kwingi mara ujitia dole.
 265. Mcheka kilema hafi bila kumpata.
 266. Mchele mmoja mapishi mengi.
 267. Mchelea mwana kulia hulia yeye..
 268. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
 269. Mcheza kwao hutuzwa.
 270. Mcheza na tope humrukia.
 271. Mchezea mavi, hayaachi kumnuka.
 272. Mchezea zuri, baya humfika.
 273. Mchimba kisima hungia mwenyewe.
 274. Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
 275. Mchuma janga hula na wakwao.
 276. Mchumia juani,hulia kivulini.
 277. Mdharau biu, hubiuka yeye.
 278. Mdharau mwiba humchoma.
 279. Meno ya mbwa hayaumani.
 280. Mfa maji haachi kutapatapa.
 281. Mfa maji hukamata maji.
 282. Mficha uchi hazai.
 283. Mfinyazi hulia gaeni.
 284. Mfuata nyuki hakosi asali.
 285. Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
 286. Mgaagaa na upwa hali ugari kande.
 287. Mganga hajigangi.
 288. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
 289. Mgeni ni kuku mweupe.
 290. Mgeni njoo mwenyeji apone.
 291. Mgomba haushindwi na mkunguwe.
 292. Mgonjwa haulizwi uji.
 293. Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo.
 294. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
 295. Mjinga mpe kilemba utamuona mwendowe.
 296. Mjumbe hauawi.
 297. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
 298. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
 299. Mkamia maji hayanywi.
 300. Mkamia maji hayanywi.
 301. Mkataa la mkuu huvunjika guu.
 302. Mkataa wengi ni mchawi.
 303. Mkataa ya Musa hupata ya Firauna.
 304. Mke ni nguo, mgomba kupalilia.
 305. Mkono moja hauchinji ng’ombe.
 306. Mkono moja haulei mwana.
 307. Mkono mtupu haulambwi.
 308. Mkono usioweza kuukata,ubusu.
 309. Mkosa kitoweo humangiria.
 310. Mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu.
 311. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
 312. Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
 313. Mla cha uchungu na tamu hakosi.
 314. Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekea.
 315. Mla mbuzi hulipa ngombe.
 316. Mla mla leo mla jana kala nini?
 317. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
 318. Mlala na maiti haachi kulia lia.
 319. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
 320. Mlimbua nchi ni mwananchi.
 321. Mnyamaa kadumbu.
 322. Mnywa maji kwa mkono mmoja,Kiu yake i pale pale.
 323. Moja shika, si kumi nenda urudi.
 324. Moto hauzai moto.
 325. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
 326. Mpanda ngazi hushuka.
 327. Mpanda ovyo hula ovyo.
 328. Mpemba akipata gogo hanyii chini.
 329. Mpemba hakimbii mvua ndogo.
 330. Mpende akupendae asiyekupenda achana naye.
 331. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
 332. Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.
 333. Msafiri kafiri.
 334. Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
 335. Msasi haogopi mwiba.
 336. Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake.
 337. Msema pweke hakosi.
 338. Mshika kisu, hashiki makalini.
 339. Mshale kwenda msituni haukupotea.
 340. Mshoni hachagui nguo.
 341. Msi bahati, habahatishi.
 342. Msi mbele, hana nyuma.
 343. Msishukuru mja, hamshukuru Molawe.
 344. Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
 345. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
 346. Mstahimilivu hula mbivu.
 347. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
 348. Mtaka lake hasindwi.
 349. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
 350. Mtaka unda haneni.
 351. Mtaka uzuri hudhurika.
 352. Mtaka yote hukosa yote.
 353. Mtegemea nundu haachi kunona.
 354. mtegemea nundu, haachi konona.
 355. Mtego bila ya chambo, haunasi.
 356. Mtembezi hula miguu yake.
 357. Mteuzi heshi tamaa.
 358. Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
 359. Mtondoo haufi maji.
 360. Mtoto akililia wembe mpe.
 361. Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
 362. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
 363. Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
 364. Mtu hujikuna ajipatapo.
 365. Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi amekulani.
 366. Mtumai cha ndugu hufa masikini.
 367. Mtumi wa kunga haambiwi maana.
 368. Mtumikie kafiri upate mradi wako.
 369. Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
 370. Muhitaji khanithi walau kana rijaali.
 371. Muiba yai leo kesho hua mwizi wa ng’ombe.
 372. Mume wa mama ni baba.
 373. Mungu hamfichi mnafiki.
 374. Mungu si asumani.
 375. Muonja asali haonji mara moja.
 376. Muuza sanda, mauti kwake harusi.
 377. Mvua nguo, huchutama.
 378. Mvumbika changa hula mbovu.
 379. Mvumbika pevu hula mbivu na mvumbika changa hula mbovu.
 380. Mvungu mkeka.
 381. Mvunja nchi ni mwananchi.
 382. Mvuvi ajuwa pweza alipo.
 383. Mwacha asili ni mtumwa.
 384. Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
 385. Mwamini Mungu si mtovu.
 386. Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
 387. Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
 388. Mwana simba ni simba.The child of lion is a lion.
 389. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
 390. Mwana wa mtu ni kizushi, akizuka, zuka naye.
 391. Mwanga mpe mtoto kulea.
 392. Mwangaza mbili moja humponyoka.
 393. Mwanzo kokochi mwisho nazi.
 394. Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
 395. Mwanzo wa ngoma ni lele.
 396. Mwapiza la nje hupata la ndani.
 397. Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
 398. Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota.
 399. Mwenda mbio hujikwa kidole.
 400. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
 401. Mwenda pole hajikwai.
 402. Mwenda wazimu hapewi panga.
 403. Mwenda wazimu hapoi, bali hupata nafuu.
 404. Mwenye haja hwenda chooni.
 405. Mwenye kelele hana neno.
 406. Mwenye kovu usidhani kapowa.
 407. Mwenye kubebwa hujikaza.
 408. Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
 409. Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
 410. Mwenye macho haambiwi tazama.
 411. Mwenye mdomo hapotei.
 412. Mwenye nguvu mpishe.
 413. Mwenye njaa hana miko.
 414. Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
 415. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
 416. Mwenye shoka hakosi kuni.
 417. Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
 418. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
 419. Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.
 420. Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
 421. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.
 422. Mwomba chumvi huombea chunguche.
 423. Mwosha hadhuru maiti.
 424. Mwosha huoshwa.
 425. Mwosha husitiri maiti.
 426. Mzaha,mzaha, mara hutumbuka usaha.
 427. Mzazi haachi ujusi.
 428. Mzigo usiouweza unaubebea nini?
 429. Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi.
 430. Mzika pembe ndiye mzua pembe.
 431. Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
 432. Mzowea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi.
 433. Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
 434. Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
 435. Nani kama mama?
 436. Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona.
 437. Nazi haishindani na jiwe.
 438. Nazi mbovu harabu ya nzima.
 439. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
 440. Ndege mwigo hana mazowea.
 441. Ndevu sio shani, hata beberu anazo.
 442. Ndugu chungu, jirani mkungu.
 443. Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
 444. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
 445. Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
 446. Ngoma ivumayo haidumu.
 447. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
 448. Ngoma ya kitoto, haikeshi.
 449. Ng’ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
 450. Ng’ombe haelemewi na nunduye.
 451. Ngombe wa Maskini hazai.
 452. Ngozi ivute ili maji. ( Udongo upate uli maji )
 453. Nguo ya kuazima, Haistiri matako.
 454. Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
 455. Nifae na mvua nikufae na jua.
 456. Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
 457. Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili.
 458. Nimerejesha kikombe na kisahani chake.
 459. Njia ya muongo fupi.
 460. Njia ya mwongo ni fupi.
 461. Njia ya siku zote haina alama.
 462. Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga.
 463. Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
 464. Nyani haoni kundule.
 465. Nyimbo mbaya haibembelezewi mtoto.
 466. Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.
 467. Nyongeza huenda kwenye chungu.
 468. Nyota njema huonekana asubuhi.
 469. Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
 470. Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
 471. Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu. (Jihadi ya nzi, kufa kidondani)
 472. Ondoa dari uwezeke paa.
 473. Pabaya pako Si pema pa mwenzako.
 474. Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
 475. Painamapo ndipo painukapo.
 476. Paka akiondoka, panya hutawala.
 477. Paka hakubali kulala chali.
 478. Paka hashibi kwa wali, matilabaye ni panya.
 479. Paka wa nyumba haingwa.
 480. Panapo wengi hapaharibiki neno.
 481. Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
 482. Pele hupewa msi kucha.
 483. Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
 484. Penye kuku wengi usimwage mtama.
 485. Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
 486. Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi.
 487. Penye miti hakuna wajenzi.
 488. Penye nia pana njia.
 489. Penye urembo ndipo penye urimbo.
 490. Penye wazee haliharibiki neno.
 491. Penye wengi pana mengi.
 492. Penye wengi pana Mungu.
 493. Pilipili usoila, wewe inakuwashia nini?
 494. Pole pole ndio mwendo.
 495. Pwagu hupata pwaguzi.
 496. Radhi ni bora kuliko mali .
 497. Radhi za wazee, ni fimbo.
 498. Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
 499. Sahau ni dawa ya Waja.
 500. Samaki mmoja akioza, huoza wote.
 501. Samaki mpinde angali mbichi.
 502. Shida haina hodi.
 503. Shida huzaa maarifa.
 504. Shika! Shika! na mwenyewe uwe nyuma.
 505. Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
 506. Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
 507. Si kila king’aacho ni dhahabu.
 508. Si kila mwenye makucha huwa simba.
 509. Si Mungu mtupu na mkono wa mtu.
 510. Sikio halilali na njaa.
 511. Sikio halipwani kichwa. (Sikio halipiti kichwa).
 512. Sikio Ia kufa halisikii dawa.
 513. Siri ya mtungi aijuaye ni kata.
 514. Sitaacha kula mkate kwa kuogopa kiungulia.
 515. Siku njema huonekana asubuhi.
 516. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
 517. Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza.
 518. Siku za mwizi, arubaini.
 519. Simba mwenda kimya (pole) ndiye mla nyama.
 520. Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
 521. Sio shehe bali ni shehena.
 522. Siri ya maiti aijuaye muosha.
 523. Sitafuga ndwele na waganga tele.
 524. Sitapiki nyongo harudi haramba.
 525. Subira ni ufunguo Wa faraja.
 526. Sumu mpe paka, mbuzi utamdhulumu.
 527. Sumu ya neno ni neno.
 528. Tabia ni ngozi ya mwili.
 529. Tamaa mbele, mauti nyuma.
 530. Taratibu ndio mwendo.
 531. Tawi kavu kuanguka si ajabu.
 532. Teke Ia kuku halimuumizi mwanawe
 533. Tonga si tuwi
 534. Tunda jema halikawii mtini.
 535. Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
 536. Ujuzi hauzeeki.
 537. Uchungu wa mwana, aujue mzazi.
 538. Udongo uwahi ungali maji (Udongo upate uli maji)
 539. Udugu wa nazi hukutania chunguni (Udugu wa nazi hukutana pakachani)
 540. Uji hajauonja, tayari ushamuunguza
 541. Ukenda kwa wenye chongo, fumba lako jicho.
 542. Ukimpa shubiri huchukua pima.
 543. Ukimuiga tembo kunya, utapasuka Makalio.
 544. Ukimwamsha alolala utalala weye.
 545. Ukinyofoa mnofu, ukumbuke kuguguna mfupa.
 546. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
 547. Ukiona moshi, chini kuna moto.
 548. Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
 549. Ukiona vinaelea, vimeundwa.
 550. Ukiona zinduna, na ambari iko nyuma.
 551. Ukistahi mke ndugu, huzai nae.
 552. Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
 553. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliye nona.
 554. Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako.
 555. Ukiujua wa mbele, nina ujua wa nyuma.
 556. Ukupigao ndio ukufunzao.
 557. Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
 558. Ulimi hauna mfupa.
 559. Ulimi unauma kuliko meno.
 560. Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo.
 561. Ulivyoligema, utalinywa.
 562. Umeadimika kama la jogoo.
 563. Umegeuka mung’unye waharibika ukubwani.
 564. Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
 565. Umekuwa bata akili kwa watoto?
 566. Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
 567. Umeruka mkojo unakanyaga mavi.
 568. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
 569. Unajenga kwa mwenzio na kwako kunaporomoka!!
 570. Unakuja juu kama moto wa kifuu.
 571. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
 572. Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
 573. Ushikwapo shikamana (Ukibebwa usijiachie).
 574. Usiache kunanua kwa kutega.
 575. Usiache mbachao kwa msala upitao.
 576. Usiache tawi kabla ya kushika tawi.
 577. Usiandikie mate na wino ungalipo
 578. Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
 579. Usijifanye kuku mweupe.
 580. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno
 581. Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
 582. Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
 583. Usiniache njia panda.
 584. Usinikumbushe kilio matangani.
 585. Usinipake mafuta kwa nyuma ya chupa.
 586. Usinivishe kilemba cha ukoka.
 587. Usione simba kapigwa na mvua.
 588. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
 589. Usisafirie nyota ya mwenzio.
 590. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
 591. Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu.
 592. Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
 593. Usitukane wakunga na uzazi ‘ungalipo.
 594. Utakosa mtoto na maji ya moto.
 595. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
 596. Utaula na chua kwa uvivu wa kuchagua.
 597. Vita havina macho.
 598. Vita si lele mama.
 599. Vita vya panzi, neema ya kunguru
 600. Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba
 601. Wache waseme.
 602. Wafadhilaka wapundaka.
 603. Wagombanao ndio wapatanao.
 604. Watu wanahisabu nazi, wewe unahisabu makoroma.
 605. Wapiganapo tembo wawili ziumiazo ni nyasi.
 606. Watetea ndizi, mgomba si wao.
 607. Wazuri haweshi.
 608. Wema hauozi..
 609. wengi wape.
 610. Zinguo la mtukufu, ni ufito

 

Methali hizi zilitumwa kwenye mojawapo ya makundi niliyomo- na hakukuwa na nukuu yoyote juu ya matayarishaji yaani aliyezikusanya methali hizi kwa pamoja- nikaona ni vema nikiziweka kwenye WordPress yangu ili kwa yoyote atakayezihitaji kuzitumia basi zikamnufaishe na aweze naye kuzitumia kwani ni kwa ajili yetu sote.

 

ASANTENI SANA.

 

TATHMINI JUU YA FURSA KWA VIJANA

WechatIMG562

Kwa majina naitwa Victoria Mwanziva, kwa sasa nasoma Nchini China; nasomea Masters ya Public Administration; Nikiwa na focus kwenye Maendeleo na Nishati (hii ndio “Thesis” Paper yangu); lakini pia kwa vile nasomea China, ninasoma sana masuala ya Kimaendeleo ya China na zaidi ya yote; masuala ya Mahusiano baina ya China na Afrika/Tanzania kiujumla.

Hii imenisaidia sana hadi sasa kufahamu kiundani masuala tambuka yanayohusiana na masuala ya Kimaendeleo. Kwa sasa huku China ninahudumu pia kama Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Jumuiya za Watanzania wanaosoma China (TASAFIC)- yaani umoja wetu wa Watanzania tunaosoma China.

Ni takribani mwaka tokea nije China kimasomo na ndani yam waka huu wa kuwa huku Kimasomo, nimejikuta nashiriki katika mambo mengi mazuri na makubwa sana; mojawapo ya vitu ambavyo vimekuwa kipaumbele kwangu ni kushiriki kikamilifu katika kuchangamkia Fursa mbalimbali zinazotangazwa kwa Nchi hii ya China, mojawapo ya nguzo zangu kuu zinazoniongoza ni pamoja na kuhakikisha nafuatilia fursa hizi kwa umakini lakini zaidi ya yote nathubutu “kuzi-apply” yaani nathubutu kuziomba hata kama nikiona ni kubwa mno ila lengo ni kuhakikisha kuwa katika kusoma kwangu, siishii kusoma tu na kupata cheti na kurudi nyumbani.

Mojawapo ya vitu ambavyo vimenisaidia kuzipata fursa hizi ni kwanza kuwa na muendelezo wa aina ya maisha niliyokuwa naishi kwa Tanzania ambayo ni kufuatilia fursa mbalimbali. Degree yangu ya Kwanza nilisomea Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam ambapo nilisomea Bachelors in Arts in Political Science and Public Administration, nilihitimu 2015.

Na katika kusoma kwangu hapo nilikuwa mwanachama hai na kiongozi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa YUNA-Tanzania ambapo nakumbuka kushiriki kikamilifu midahalo, makongamano, semina, warsha mbalimbali jengefu kwa ngazi mbalimbali yaani kama muandaaji, muwezeshaji, mshereheshaji na kadhalika.

Hapa najaribu kukujengea picha kwamba hii ni safari, safari ambayo nilianza muda mrefu sana- kwanzia Sekondari, hata Shule ya Msingi- ni safari ndefu ya kuwa na kiu cha kujifunza, kuwa  na ari na hamasa ya kufikia sehemu fulani ila zaidi ya yote kuhakikisha kwamba uwepo wangu unakuwa wa manufaa kwa jamii inayonizunguka sana sana vijana wenzangu ambao wananizunguka.

FURSA

Fursa ninazozungumzia mimi nyingi ni zile jengefu zinazomjenga kijana aweze kujipambanua, kujitambua, kuongeza upeo na maarifa ambayo ni chachu ya yeye kufikia malengo yake haswa ya kitaaluma, kikazi. Naamini wengi safari yetu ni moja ya kutafuta kujitegemea na kuhakikisha kuwa tunakuwa msaada kwa familia na jamii zetu, ila safari hiyo ili uifikie lazima kuna hatua uzipitie na kama utawekeza katika kujijenga na kujinoa basi bila shaka safari hiyo itakuwa ni yenye manufaa kwako kwa maana ya kukufanya uithamini na utambue umuhimu wa kila hatua unayopitia kama kijana.

Kila mmoja wetu anapitia vitu mbalimbali ambavyo vinamfanya awe alivyo; ila naamini matukio mengine tukiyakadiria na tukijiandaa nayo basi matokeo yake yatatabirika na kuweza kuleta ile picha ya kwamba huyu mtu atakuja kuwa mtu wa aina gani. Hapa namaanisha kwamba; kijana akiwekeza muda wake katika kujifunza na kujipambanua kwa kufuatilia kwa makini vitu ambavyo vitamjenga, basi tunajua kabisa kwamba mwisho wa siku huyu Kijana atakuwa ni wa aina gani- atakuwa kijana makini, anayejitambua, anayetambua mazingira yake na anayetambua umuhimu wa kujituma na kujitolea.

WechatIMG561

FURSA KWA VIJANA:

Fursa kwangu mimi ni mwanzo mpya, ni kitu ambacho kinaweza kikamtoa mtu katika hatua moja na kumpeleka katika hatua nyingine.

Namna kuu ya kuzipata fursa mbalimbali:

 • Kuwa mfuatiliaji wa masuala tambuka; yaani kuwa na ile hamasa na ari ya kufahamu vitu vingi kwa kufuaitilia taarifa za nchini nan je ya nchi kupanua wigo wako wa uelewa wa mwenendo wa kidunia na kitaifa
 • Kuwa na utayari kujifunza; unapoamua kufuatilia Fursa lazima uwe tayari kujifunza na hakikisha unasema dhahiri kwamba “nahitaji kujua zaidi, nahitaji kujifunza zaidi”
 • Shirikiana na vijana wenzako, naamini katika kujenga mtandao na kuambatana na watu mnaowaza vitu vinavyoendana; unapofungua wigo wako wa watu wanaokuzunguka hakikisha unakuwa tayari kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali na jenga ukaribu na watu unaotamani kujifunza kutoka kwao
 • Kuwa na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii, Mitandao ya kijamii ni chanzo kikuu cha taarifa za fursa mbalimbali hakikisha unajipambanua katika matumizi yako ya mitandao ya kijamii ili uweze kufikia malengo yako ya kufuatilia fursa mbalimbali
 • Hakikisha unafuatilia kurasa zinazohamasisha na kutoa taarifa zinazohusiana na fursa mbalimbali- yaani tahadhari sana na aina ya “content” unayoingiza akilini mwako hakiksha unasoma na una-focus katika vitu jengefu na wezeshi ili uweze kufikia malengo yako
 • Jitahidi uwe daraja la kufikisha taarifa za fursa kwa wenzako, yaani usikae ukategemea msaada kila siku jitahidi wewe usaidie angalau hata mtu mmoja au wawili kufikia malengo yao ili uweze kuwa mwenye msaada kwa jamii yako- hii ni rahisi kutokana na urahisi wa matumizi wa mitandao na urahisi wa kufikisha taarifa hizi kupitia makundi ya Whatsapp, Mitandao ya Kijamii kama Twitter na Instagram nk
 • Jitahidi kutumia talanta, muda, kipaji na nyenzo nyinginezo kukusaidia kufika unapotamani kufikia; mojawapo ya vitu muhimu ni kuhakikisha kwamba unajituma na unatumia kipawa chako kutimiza malengo yako. Vijana wengi tumekumbwa na wimbi la kutokuthamini tulivyonavyo ila kuangalia tusivyonavyo kitu ambacho kinaturudisha nyuma- embu jitathmini yale yote mazuri uliyonayo na mawazo na fikra nzuri ulizonazo- ukiamua kujituma na kuthubutu kuzifanyia kazi basi bila shaka utafikia malengo yako.
 • Jipe moyo na Jitume- usikae ukategemea atakuja mtu kukufanyia kazi na kukuwezesha lazima ujiwezeshe uoneshe nia kabla ya kutegemea kufika mahala fulani, jitihada zako binafsi zinapaswa kukupa nguvu na kuwa ngazi yako ya kufikia malengo yako.
 • Soma sana, Jifunze kusoma Vitabu, Makala, Magazeti, Majarida na aina yoyote ya material wezeshi, elekezi, zinazofundisha na zinazokuinua na kukutafakarisha ili uweze kufikia malengo yako katika jamii kiujumla- kusoma kunasaidia sana kumfungulia mtu upeo na dunia yake kiujumla.

WechatIMG563

FURSA ZA KIMATAIFA KWA VIJANA:

Fursa za kimataifa ni zile fursa ambazo kijana anaweza akapata kuweza kushiriki aidha Semina, Mikutano, Mashindano, Warsha, Mafunzo na kadhalika katika nchi nje ya ile anayoishi. Haya pamoja na mengineyo kama Biashara, Michezo, Elimu zinazopatikana nje zote ni fursa za kimataifa zinazopatikana kwa vijana wakiamua kuzifuatilia.

Mimi katika Nyanja ya kimataifa nimejitahidi nikiangalia na umri wangu wa Miaka 26, tayari nimekwishatembelea nchi kadha wa kadha Duniani kupitia ufuatiliaji wa fursa hizi za kimataifa ambazo mara zote gharama zote zinakuwa juu ya taasisi, shirika au nchi inayokualika.

Kikubwa kinachohitajika ni ufuatiliaji na umakini katika kujituma na kujitolea kufuatilia fursa mbalimbali, fursa hizi zinapatikana kwa wingi na nimekuwa mmoja wa vijana ambao tupo mstari wa mbele kuzisambaza kwa vijana wenzetu ili wao pia wazifuatilie na wajifunze kutokana na fursa hizi. Ili wao nao wanufaike nazo, sio tu kwa manufaa yao binafsi, bali kwa manufaa ya taifa zima.

Fursa za kimataifa zipo nyingi sana, na zimejigawa katika Nyanja tofuati tofauti- kwa vijana walioamua ku-focus katika nyanja hizo- mfano vitu kama Mahusiano ya Kimataifa; kupitia fursa zinazopatikana Umoja wa Mataifa nk, Fursa za Kiuchumi, Biashara, Elimu, Afya na mengineyo mengi. Ila suala kuu linalokuja hapa ni ufuatiliaji na  kujiwekeza muda wako katika kufuatilia na kujidhatiti katika kufuatilia.

Mojawapo ya nguzo kuu za kuzipata fursa hizi za Kimataifa ni kujijenga kwanza ili CV yako iwe nzuri, na yenye uzito na hii inaanzia nyumbani ulipo kwa kuhakikisha unakuwa mfuatiliaji na mstari wa mbele katika kujipambanua kifikra.

Uandishi ni sehemu muhimu ya kupata fursa kwani itakubidi ujielezee na uweze kuelezea vema unachofanya, ulichofanya na unachotarajia kufanya katika kuipata fursa hiyo. Mojawapo ya nguzo kuu ni kuhakikisha unaweka rekodi zote za muhimu za kazi zako, za hatua zote unazopiga sio kwa dakika ya mwisho ndio uanze kushika hapa na pale. Napendekeza mumfuatilie Kelvin Mwita ni mhadhiri kijana ambaye anaelekeza sana namna bora ya kuandika CV, na kuweka sawa rekodi zako na namna ya kuziomba fursa mbalimbali.

Ningependa nitaje vijana wengi wa Kitanzania wanaofanya vema katika nyanja za kimataifa ila kwa toleo lijalo, kwa leo nimegusia tu umuhimu wa kufuatilia fursa hizi na kuthubutu kuziomba fursa hizi- ukishiriki mikutano ya kimataifa unaweza ukajionea namna ambavyo vijana wa nchi mbalimbali ushiriki wao unavyokuwa mkubwa zaidi na mwingi zaidi- moja ya sababu ni kuchangamka katika kuzifuatilia na kujipanga katika application wazifanyazo. Ila kikubwa zaidi wanazifanya application hizi mara kwa mara bila kuchoka na kwa kujituma kweli kweli ili waweze kuongeza uwezekano wao wa kuzipata fursa hizi.

Kwa kuhitimisha- Fursa zipo nyingi na binafsi nimekuwa mnufaika wa fursa hizi kutokana na ufuatiliaji na kujituma, hata kwa hapa nilipo China nimeendelea kujituma na kuzichangamkia fursa; kwa muda mchache nilioweza kuwa hapa nimejitathmini na nimejipambanua katika, masuala ya Belt and Road Beijing, niliposhiriki kwenye Forum ambayo ilinipa tuzo ya Muwasilishaji mada bora, Nilishiriki katika Mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa jijini Shanghai ambapo pia nilishinda tuzo ya muwasilishaji mada bora, juzi nimetunukiwa tuzo ya moja ya Makala bora kutoka chuo cha Sichuan, Chengdu niliposhiriki mashindano ya Uandishi wa Makala zinazoelezea ushirikiano kati ya Afrika na China. Lakini pia nimeweza kushiriki Mkutano Mkubwa wa Vijana Hangzhou, Zhejiang ulioratibiwa na Jack Ma (Alibaba) ambapo tulipewa semina maalumu ya maendeleo kwa vijana- pamoja na semina nyinginezo nyingi hapa mjini kwangu nnaposoma Harbin. Kitu kinachofanana juu ya fursa hizi zote ni kwamba zilinifikia mtandaoni yaani kupitia Makundi ya Wechat, na Mitandao ya Kijamii.

WechatIMG571

Ninapenda kuwa muwazi kuwa sio kila fursa utakayoomba utaipata, ila kila fursa itakayoifuatilia na kuichangamkia itakufundisha namna bora ya kufuatilia fursa itakayofuata. Kuzidi kuomba fursa na kufanya application mbalimbali kutakufundisha namna bora ya kuiomba inayofuata, ila zaidi ya yote jitahidi kujiweka katika nafasi ya kujifunza na kuwainua wenzako kupitia kujifunza huko.

 

WENU

VICTORIA MWANZIVA

 

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA SHIRIKISHO LA JUMUIYA ZA WANAFUNZI WA KITANZANIA WANAOSOMA NCHINI CHINA (TASAFIC) SHENYANG, LIAONING. 1- DESEMBA-2018

Mkutano mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi Watanzania nchini China ulifanyika mjini Shenyang, Liaoning tarehe moja Disemba (01 /12) kwa mwaka 2018. Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania mjini Shenyang ilipata nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo kikuu cha uhandisi wa masuala ya anga (Shenyang Aerospace University)

Mkutano huu ulipata bahati ya kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa. Mbelwa Kairuki kama mgeni rasmi akiambatana na Afisa mwandamizi wa Ubalozi Bwana Lusekelo Gwassa (Kaimu Mwambata wa Elimu na Fedha).

WechatIMG796

Mbali na ugeni huo, mkutano huu pia ulihudhuriwa na wageni waalikwa ambao walikuwa Walimu wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Petroli na Gesi Liaoning (Liaoning University of Petroleum and Gas), Wawakilishi wa vyuo vingine vya Jimbo la Liaoning, Wakurugenzi wa Kampuni wakala wa masomo ya nje ya nchi (Global Education Link) Bwana Abdul Mollel na Bi. Zakia Mollel.

Aidha Kamati Tendaji ya Shirikisho la Jumuiya za Watanzania Wanaosoma China TASAFIC iliwakilishwa na Mwenyekiti Bw. Dennis Mukama na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bi. Victoria Mwanziva.

Mkutano huu ulileta pamoja Viongozi wawakilishi na wajumbe kutoka katika miji mbalimbali Nchini China ambapo kuna Jumuiya za Watanzania wanaosoma katika miji hiyo (mwisho wa taarifa hii kuna kielelezo cha uwakilishi wa kila Jumuiya)

WechatIMG540.jpeg

 

MAUDHUI

Mkutano ulibeba ajenda mbalimbali kutoka meza kuu pamoja na maswali na maoni kutoka kwa wanafunzi wahudhuriaji. Ajenda hizo ziligusa maeneo kama afya ikiwa ilikuwa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, Fursa za kiuchumi, Fursa za udhamini wa masomo pamoja na sheria na utaratibu wa namna ya kuishi nchini China bila kusahau umoja na mshikamano baina ya Watanzania. Mpangilio na wahusika wa maudhui ulikuwa kama ifuatavyo.

UFUNGUZI WA MKUTANO

Muongozaji wa Mkutano Bi.Victoria Charles Mwanziva (Makamu Mwenyekiti TASAFIC) alifungua mkutano kwa kuwakaribisha ukumbini mgeni rasmi Mheshimiwa. Balozi aliyeambatana na Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini China Ndugu Lusekelo Gwasa pamoja na viongozi wa Jumuiya zote shiriki na wajumbe wote kiujumla. Baada ya ukumbi kuimba wimbo wa taifa ulifuata utambulisho wa kila muhudhuriaji hadi kufikia meza kuu.

SALAMU KUTOKA KWA WENYEJI (BI. RACHEL KAALI)

Bi. Rachel Kaali Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania Shenyang aliwasilisha salamu zao kwa mgeni rasmi na wanachama wa TASAFIC, Mwenyekiti aligusia maeneo mbalimbali ikiwemo historia fupi ya Jumuiya hiyo na namna ambavyo imeweza kuwaleta Watanzania pamoja kwa njia mbalimbali kama kuanda sherehe hasa sherehe ya maadhamisho ya kumbukumbu ya uhuru ambapo tumeona miaka yote watanzania wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakishiriki kwa pamoja kusherehekea siku hii ya muhimu kwa taifa letu na hivo kudumisha umoja na mshikamano kati yao.

Kumekuwa na utaratibu wa kukisaidiana kukiwa na shida na adha mbalimbali wawapo masomoni kama vile magonjwa, kupotea kwa passport ama wakiwa na shida mavyuoni mwao. Kwa namna moja ama nyingine wameweza kusaidiana kama watu wa taifa moja kwa michango, kutembeleana na kushauriana kama Watanzania wanaosoma Shenyang.

Shenyang pia wamefanikiwa kuiwakilisha nchi yetu ya Tanzania katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo na shughuli za kila siku mavyuoni mwetu hivo kuonesha uhai wetu kama watu wa taifa kubwa na linaloendelea. Katika masomo jumuiya hiyo imepiga hatua kubwa sana ambapo kwa miaka yote zaidi ya asilimia 95 Watanzania waliokusidiwa kuhitimu katika vyuo mbalimbali wamekuwa wakifanya hivo kwa muda sahihi, pamoja na hili watanzania wengi wamekuwa wakichukua kwa wingi tunu mbalimbali zinazotolewa mavyuoni mwao katika masomo.

Bi. Racheal alielezea baadhi ya Changamoto ambazo ziligusia suala la ufuatiliaji na kusaidika pale mwanafunzi anapopoteza pasipoti na masuala mbalimbali ya kiutaratibu. Pili; alihimiza umuhimu wa upatikanaji wa taarifa sahihi na muhimu za kujiendeleza kama wanafunzi Watanzania nchini China. Mwisho aliwakaribisha sana wajumbe wote mkutanoni na kushukuru ujio wao wote

 

TAARIFA YA TASAFIC (MKT.DENIS MUKAMA)

Mwenyekiti wa TASAFIC Bwana Dennis Mukama alifuatia kwa hotuba fupi iliyoainisha changamoto na mafanikio ya TASAFIC. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na muitikio hafifu wa wanafunzi wanaojilipia ada wenyewe (non-scholarship) kuwa mbali na shughuli za shirikisho. Changamoto nyingine ni wanafunzi wanachama kulalamika kutapeliwa ama kudhulumiwa na baadhi ya mawakala wa elimu ya juu ya nje.

Mwenyekiti pia hakuacha mafanikio ya TASAFIC yakose mzungumzaji, alibainisha wazi jitihada zinazofanywa na shirikisho kuhakikisha ustawi mzuri wa jamii ya Watanzania nchini China ikiwemo ushirikishwaji katika taarifa za fursa za kimasomo ambao katika eneo hilo shirikisho limeunda kikosi kazi na kundi maalumu la kusimamia wanafunzi wanaokuja kusoma China kuanzia hatua za mwanzo za kupata taarifa sahihi hadi wanapofikia maeneo yao ya kuishi na kusoma.

Kwa kipindi cha mwaka mmoja shirikisho limeweza kukusanya zaidi ya watanzania 3000 kutoka nyumbani pamoja katika makundi ya kupeana taarifa za udhamini wa kimasomo, katika nafasi 1000 za masomo shirikisho limeweza kusaidia wanafunzi 150 kuweza kupata nafasi hizo lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi hadi kufikia 6000 kwa mwaka huko mbeleni.

Kwa kuhitimisha Mwenyekiti Mukama alitumia nafasi hii kumualika jukwaani Engineer Nicas Bernard (Mwenyekiti Tianjin) ambaye ni mmoja wa wana-team wa program hii ya scholarship kwa Watanzania, na Eng Nicas  akasalimia na kushukuru sana muamko na muitikio wa Watanzania na akashukuru sana Wana-Team wote kwa kujitolea kwao na akahakikisha kazi itaendelea kuwanufaisha Watanzania juu ya fursa za kimasomo Nchini China.

AFISA WA UBALOZI (MWAMBATA WA ELIMU) BW. LUSEKELO GWASSA

Mwenyekiti wa TASAFIC alimkaribisha afisa wa ubalozi Bwana Lusekelo Gwassa ili aweze sema neno kidogo kwa wahudhuriaji kabla ya kumkaribisha Mheshimiwa Balozi.

Afisa alianza kwa kutolea ufafanuzi wa taratibu na namna ofisi ya ubalozi inavyofanya kazi ili kuepusha changamoto za usafiri na malazi kwa wale wanaotoka mbali na kufuata huduma za ubalozi Beijing.

Baada ya hapo alielezea umuhimu wa kufuata sheria na utaratibu wa nchi ili kuweza kujiepusha na misuguano na mamlaka za uongozi za serikali ya China. Wanafunzi pia wameaswa kuepuka makundi yasiyo na tija yaliyojaa tamaa za kimaisha kwani sio mara moja au mbili wanafunzi wamekuwa wakijikuta mikononi mwa vyombo vya ulinzi na sheria China kwa kudhamiria au pasipo kudhamiria.

Ndg. Gwassa aliweka wazi aina ya kesi za madawa ya kulevya ambazo zimepelekea baadhi ya watanzania kufungwa nchini huku bila msaada wowote kutoka kwa ndugu zake kwani mamlaka haziruhusu kutembelea watuhumiwa hata mahabusu. Watoto wa kike pia wamekumbushwa kuacha kujishughulisha na makundi yanayopeleka wao kujikuta katika biashara za kujiuza kwa wafanyabiashara kwa kigezo cha wafanyabiashara kutafuta wakalimani. Hili limepelekea hadi baadhi kujikuta na maambukizi ya magonjwa kama UKIMWI.

Ndg Gwassa alitumia nafasi hiyo kupongeza jitihada za Viongozi wa Jumuiya Mbalimbali kuendelea kushirkiana vema na ubalozi katika kuwasilisha project; initiatives mbalimbali zenye malengo ya kuinua nchi ya Tanzania.

WechatIMG787

 

 

UWAKILISHI WA GLOBAL EDUCATION LINK (GEL) BW. ABDULMALICK MOLLEL

Kabla ya kumkaribisha Mhe. Balozi, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link kampuni wakala wa elimu ya juu vyuo vya nje alipata nafasi ya kuzungumza naye kwa ufupi.

Bw. Mollel alieleza umuhimu wa wanafunzi kuwa wepesi kushitaki na kutoa taarifa zozote zenye kuhusiana udanganyifu, utapeli au udhulumishi wa aina yoyote unaofanywa na mtu, watu au kikundi kinachojiita wakala kwani kwa kuendelea kulalamika chini bila kuchukua hatua kunachafua taswira ya wengine wanaofanya shughuli hizo kwa uadilifu. Bw. Mollel aliweka wazi jitihada zinazofanywa na kampuni yake katika kuhakikisha suala la elimu ya nje halichukuliwi kama anasa bali fursa kama zilivyo fursa zingine zozote zile. Jitihada hizo ni pamoja na kutenga kiasi cha shilingi bilioni 6 ili kufanikisha mikopo ya elimu ya nje isiyo na riba (zero interest loans) pamoja na jitihada za kufungua ofisi ya kampuni hiyo Shenyang ambayo itaanza rasmi kazi January 2019 ili watanzania waishio China wapate huduma kwa haraka na kutoka kwa watu wanaolewana nao, huduma hizo ni pamoja na masuala ya uhamiaji, afya pamoja na changamoto za kitaaluma.

Mkurugenzi huyo hakusita pia kukemea tabia za kimaovu za kujiuza na ulevi kwa watanzania kwani zimekuwa zikiharibu hata nafasi ya ushawishi wa watanzania katika masuala mbalimbali ya kijamii na elimu.

  

MGENI RASMI MH. BALOZI MBELWA KAIRUKI (BALOZI WA TANZANIA NCHINI CHINA)

Hatimaye uliwadia muda wa mgeni rasmi Mheshimiwa Balozi kuzungumza na wahudhuriaji, Mhe.Balozi  aliweka wazi nia yake ya kuomba mkutano huu ufanyike tarehe moja Disemba siku ambayo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani. Hivyo basi suala la afya lilikuwa kifungua hotuba na moja ya mambo muhimu aliyoweza kuzungumza Mheshimiwa Balozi. Kutokana na kauli mbiu ya siku hii kuwa “jua hali yako “Mhe. Balozi aliweka wazi umuhimu wa mtu kutambua hali yake kwa kwenda kupima kwani kwa maneno ya Mhe. Balozi “Kujua hali zetu ni hatua ya kwanza muhimu ya kuchukua hatua”

Mheshimiwa Balozi Kairuki alisema; Jambo moja ambalo ni dhahiri, hivi sasa vijana wanalifanyia mzaha suala la ukimwi. Pengine niliseme kwa lugha ya kigeni ili mlipate vizuri “There are still a lot of misconceptions about HIV among young people, and young people generally tend to underestimate the risks they take”. Vijana wengi hawana taarifa za kutosha kuwapa ufahamu wa Ugonjwa wa UKIMWI. Hiyo ndio sababu iliyopelekea Kauli mbiu ya Mwaka huu kumtaka kila mmoja wetu kufahamu Hali yake. Tusiogope.

“Young people are the world’s greatest hope in the struggle against this fatal disease. Changing behaviours and expectations early results in a lifetime of benefit – both in HIV prevention and in overcoming HIV-related stigma. On this World AIDS Day, let’s stand together to reach the goal of an AIDS-free generation”. Alihitimisha Balozi Mbelwa Kairuki

Balozi pia aligusia umuhimu wa kuchangamkia fursa mbali za kiuchumi zitokazo kwa makampuni na serikali ya China, aliwakaribisha wanafunzi wageni China na kuwaasa  “Nawakaribisha wanafunzi mliokuja China kusoma kipindi hili,kipindi ambacho tunasema ni interesting times kifursa “ Mh.Balozi aliweka wazi masikitiko yake juu ya watanzania kutokuwa wepesi na haraka kuchangamkia fursa hata zile zinazoletwa mezani nyumbani, aliweka kwa mifano hai kama fursa ya kuleta tani  100,000 za maharage China amabazo hadi sasa ni tani  84 tu ndizo zilizotimia sawa na asilimia  0.084 ya kazi.

Mheshimiwa Balozi alikumbushia “Kwani miezi mitatu iliyopita, kule Beijing ulifanyika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika ambao ulitoka na maazimio na mpango kazi ambao unatoa fursa kem kem kwa bara letu. Katika kipindi cha miaka mitatu ijayo China imeahidi kuanzisha:

 1. Programu ya ujenzi wa maeneo maalum ya viwanda barani Afrika;
 2. Programu maalum ya ujenzi wa miundombinu ya nishati, usafirishaji,habari na 
mawasiliano
 3. Programu ya kukuza wigo wa biashara kati ya China na Afrika
 4. Programu ya mapinduzi ya kijani
 5. Mpango maalum wa mafunzo ya wataalam wa fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na 
mafunzo ya ufundi- hapa China imeahidi kutoa Scholarship 50,000 za mafunzo ya muda mrefu, na nafasi 50,000 za mafunzo ya muda mfupi. Vilevile, China itanzisha Kituo cha Kuendeleza Ubunifu na Ujasiriamali kwa vijana mahiri wapatao 1,000, vilevile itatoa mwaliko kwa vijana 2,000 kufanya ziara ya mafunzo nchini China.
 6. Programu ya Kuboresha Sekta ya Afya
 7. Programu Ushirikiano katika masuala ya habari, utamaduni, sanaa na michezo
 8. Programu ya Ulinzi na Usalama

Mhe. Balozi aliwakumbusha pia wanafunzi wanaofanya masomo yao ngazi ya uzamili na uzamivu kujikita katika kuandika ripoti za kiuchunguzi zenye malengo ya kutatua matatizo ya nyumbani aliweka katika maneno haya  “leo hii mbegu ya muhogo Tanzania inatoa tani 1-7, sehemu nyingine duniani mbegu hiyo hiyo inakupa hadi tani 20,wanafunzi mjikite kwenye tafiti ambazo ni relevant na matatizo ya nyumbani”

Watanzania Wanafunzi wanaosoma China- walisisitzwa kuwa raia wema na mabalozi wazuri watanzania kwenye nchi ya China. Fuateni sheria za nchi; zingatieni utamaduni wao ili msiwakwaze.

Tulikumbushwa kuwa tumekuja hapa kusoma, sio kutalii wala kufanya biashara- visa zetu ni za Masomo hivyo bidii iwe kwenye masomo. China kama ilivyo sehemu nyinyine zote kuna mambo mengi yenye ushawishi yanayoweza kukuondoa katika mstari.

Mheshimiwa Balozi alisisitizia kuwa Taifa linatutegemea, jamii inatutegemea, familia zinatutegemea na wazazi watutegemea tusome ili turudi tukasaidie ujenzi wa taifa na si vinginevyo.  Balozi Kairuki aslisistiza kuwa tuzingatie sheria za vyuo vya China. “Mzisome, mzielewe. Kutokuelewa sharia sio sababu 
ya kuvunja sharia” Alisema- ‘Igonorance of the law is not excuse’.

Mheshimiwa Balozi aligusia masuala ya Umuhimu kutunza afya zetu. “Kila mwanafunzi lazima awe na Bima ya Afya ‘comprehensive Medical insurance’ ambayo mnatakiwa kuikata kila mwaka.

Masuala ya nidhamu: “Epukeni tabia za migomo vyuoni. Hayo ni mambo ambayo hayakubaliki wala kuvumilika kwa wenyeji wetu. Kama mna issues/concerns tumieni njia sahihi za mawasiliano zilizopo vyuoni au kupitia kwa Wafadhili wenu au Ubalozi au Mawakala wenu”.

Na mwisho liliwahusu wanafunzi wa Masters na Phd. Mheshimiwa Balozi aligusia kuwa Maprofesa wanataka tufanye utafiti kwenye masuala yanayohusu nchi yetu kwenye eneo la utaalam la mwanafunzi husika. Nia yao hasa ni kuelimika na kupata ufahamu wa nchi yetu kwa malengo yenye manufaa yao. “Sasa na sisi tuhakikishe kwamba utafiti tutakaoufanya uwe ni ule wenye tija na manufaa kwa nchi yetu na sisi tuvune elimu na Maarifa yao kwa faida yetu”.  Alimalizia kwa kusema “Your research should be oriented towards solving the problems of tanzania-as they are, and as they can reasonably be expected to be in the future”

“Kama wewe ni mtaalam wa kilimo kafanye utafiti wa kupata suluhu ya changamoto ya ugonjwa wa korosho au kahawa au migomba ili matokeo ya kazi yako yakasaidie kutatua matatizo halisi yaliyopo nyumbani” Alihitmisha kwa kuwatakia kila la kheri wajumbe wote katika masomo yao.

Mhe Balozi alitambua kazi nzuri iliyofanywa na TASAFIC- kupitia Programu yao ya ‘HIGHER EDUCATION OPPORTUNITIES IN CHINA FOR TANZANIANS’. TASAFIC kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa Watanzania juu ya fursa za MASOMO NA UFADHILI wa elimu ya juu nchini CHINA. Program hiyo iliratibiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho Ndugu Remidius Mwema. Balozi Kairuki aliwataja wote waliohusika katika mpango huo wa kujitolea na kuwapongeza sana kwa kazi kubwa nzuri waliyofanywa. Na akazidi kutia moyo kikosi kazi kipya cha mpango huo ambacho sasa kinaratibiwa na Katibu wa TASAFIC Ndugu Miraji Mngereza na “Team Task Force” nzima ya HEOCT.

Mheshimiwa Balozi alihitimisha kwa kutoa rai kuwa kila mtu kwa nafasi yake na uwezo wake “afanye jambo lolote la kuinufaisha nchi yetu na watu wake bila kubagua wapi tunapotoka, imani gani tunaifuata, chama kipi cha siasa tunakiamini kwasababu yote kwa yote sisi sote ni Watanzania kabla ya kitu kingine chochote”

 

WechatIMG776

 

MASWALI NA MAJIBU KUTOKA KWA WAJUMBE WA MKUTANO

Kulikuwa na muda makhususi wa Maswali na Majibu kutoka kwa washirki kuelekea meza kuu, na kwa ujumla wake maswali yaligusia masuala yafuatayo; Yaliyowasilishwa kutoka kwa washiriki wa Mkutano huu wa Watanzania wanaosoma China.

 1. Mchakato wa kupata passport mpya Wanafunzi Watanzania wakiwa bado China
 2. Utaratibu na uwezekano wa kupata vitambulisho vya uraia Wanafunzi Watanzania wakiwa bado wapo China
 3. Uwezekano wa ubalozi kuhakikisha Wanafunzi hao wanapata Internships huku China na Nyumbani
 4. Namna gani fursa za kimasoko zinapatikana kwa wanaojishughulisha na Kilimo
 5. Kuna muongozo gani wa makundi mbalimbali kutokana na taaluma ili kuweza kuzifikia fursa
 6. Masuala ya Bima za Afya kwa Wanafunzi na Changamoto zinazoambata nazo

Majibu kiujumla yaliyotoka kutoka kwa geni rasmi Balozi wa Tanzania Nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki aliyeambatana na Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini China Ndugu Lusekelo Gwasa;

 1. Masuala ya Passport yote yanashughulikiwa na Uhamiaji Makao Makuu Tanzania; na Ubalozi ndio unaosimamia zoezi hili kwa Watanzania waliopo China- usimamizi huu ni wa kiutaratibu tu na maelekezo; ila utoaji wa hati hufanyika Tanzania tu haswa sasahivi ambapo zinahitajika Biometric Data za mhusika anayehitaji Hati hizo za kusafiria.
 2. Kulikuwa na Kijana Lutfi Bathigili mwanafunzi wa Kitanzania anayesomea ‘Masters ya Nuclear Energy’ akagusia kuwa anachosomea kwa Tanzaina bado hakijawa na soko na anahitaji kupewa nafasi pate sehemu aidha ya kuweza kujifunza kwa Vitendo au hata kazi moja kwa moja katika Sekta hiyo ya Nyuklia- Mheshimiwa Blaozi alimpa Kijana huyo nafasi ya papo kwa hapo ya kuunganishwa katika Kampuni kubwa ya Masuala ya “Nuclear” amabyo inahitaji vijana wanaosomea masuala hayo- aweze pata nafasi ya internship ya kujifunza kwa vitendo juu ya utaalamu wake hapa Nchini China.
 3. Watanzania waliagizwa kutoa namba zao za simu ili wakutanishwe kwenye makundi mbalimbali ya kitaaluma maalumu yanayojihusisha na kuwaleta pamoja Wanataaluma wanaosoma China katika makundi maalumu kama vile Madaktari, Wahandisi, Wachumi na kadhalika ili waweze kupata fursa za moja kwa moja zinazohusiana na masuala ya taaluma zao- fursa hizi ni pamoja na makongamano, taarifa zinazohusu taaluma zao, taarifa za ufadhili wa masuala ya taaluma zao, taarifa za Internships na mengineyo. (Makundi haya yanaratibiwa na Katibu Mkuu wa TASAFIC Ndugu Miraji Mngereza)
 4. Kufuatilia taarifa za fursa kwenye vyombo vya taarifa vya ubalozi ikiwemo kurasa zao za mitandao ya kijamii- Baadhi ya Watanzania waliuliza masuala ya Fursa na taarifa za China; wakaelekezwa kufuatilia kurasa za kijamii za Kichina kwenye mitandao ya Kichina kwani fursa ni nyingi sana nchini China. Lakini pia kufuatilia kazi za Ubalozi kupitia ukurasa wa Ubalozi wa Twitter “Tanzanian Embassy in China”
 5. Vijana waliaswa sana kufuatilia masuala yanayowahusu hasa taarifa za kiutaratibu kama vile za Visa (Waliaswa wawe makini na masuala ya Tarehe za kuisha kwa Visa zao, na Reisdence Permit zao, pia masuala yao ya Hati za Kusafiria ili kuweza kuishi kwa kufuata Taratibu na Sheria za Nchi ya China.
 6. Mheshimiwa Balozi alisistizia sana suala la Kufuatilia Fursa za Kimataifa na nyinginezo nyingi nchini China- kama vile Makongamano, Semina, Expo-Expeditions na akamtaja Katibu Mkuu mstaafu wa TASAFIC kama moja wa mfano bora wa vijana waliokuwa wakijishughulisha na ufuatiliaji wa fursa kadha wa kadha- haswa Expeditions ili ajifunze zaidi; Akawataja pia Phelisters Wegesa- Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanasoma Henan na Victoria Mwanziva Makamu Mwenyekiti TASAFIC kama mifano bora ya vijana wanao-jitahidi kufuatilia fursa mbalimbali za kujijenga na kujiongezea ujuzi, lakini pia wamekuwa mstari wa mbele kuzisambaza kwa wenzao kupitia mitandao ya kijamii ili nao pia waweze kunifaika na fursa hizo kwa manufaa ya maendeleo ya taifa letu la Tanzania.
 7. Kulikuwa na nafasi ya Muwakilishi kutoka Global Education aliyeainisha kwa kina baadhi ya Changamoto na tatuzi zake kwa wanafunzi waliopo China na kusisitiza kuhusiana na umuhimu wa kuwa na ushirikiano baina ya Makundi ya Wanafunzi waliomo katika usimamizi wa mawakala pamoja na wanafunzi wanaojisimamia wenyewe na ambao wanasimamiwa na Scholarships mbalimbali; kwa lengo la kuhakikisha kuwa kunakuwa na mawasiliano mazuri baina ya makundi haya- na kunakuwa na ushirkiano katika uandaaji wa shughuli mbalimbali zinazowagusa watanzania hawa waliopo katika makundi mbalimbali kwani kuna taratibu maalumu za Global na ni muhimu kudumisha ushirikiano huu unaoenda kudumisha umoja baina ya makundi mbalimbali kama Watanzania wanaosoma China.

Ndugu Abdulmalick Mollel wa Global pia aligusia kwa ujuzi wake na uzoefu wake kuwa Vyuo Vikuu vya China vina usimamizi wa moja kwa moja wa Wanafunzi wanaosoma katika taasisi zao- na wanapaswa kuhusika moja kwa moja  hivyo ni suala la kuwa na ukaribu na Uongozi wa Chuo; kuwa wafuatiliaji na daima kuwa mtu wa kuulizia fursa; matukio mbalimbali ili kuweza kujiinua na kuhakikisha kuwa unakuwa na uwakilishi stahiki kwa nchi yako na future yako.

Masuala ya Bima Ndg Mollel alisisitiza kuwa kuna Bima za aina tofauti tofauti na akasisitiza kuwa kwa wanafuzi wanaojilipia wanapaswa kuhakikisha kuwa wanajilipia bima ya juu ili kuwa na full coverage na akaainisha kuwa kuna umuhimu wa kuwa na uhakika wa aina ya bima anayoenda kuingia mtu ili awe salama.

 1. Mheshimiwa Balozi alisisitizia kuwa Wanafunzi wanapaswa kuwa na mawasiliano ya Karibu na Vyuo vyao- wawe karibu na masuala ya College za International Education; yaani ofisi maalumu zinazoshughulikia masuala ya Wanafunzi wa Kimataifa ili wawe salama na wapate ushirikiano wakutosha kwa masaual yote ya kitaaluma, fursa, bima maana vyote vinahitaji ufuatiliaji wa karibu na ufuatiliaji huo utatokana na kujituma na kujishughulisha kwa wanafunzi husika ambao wanasoma katika taasisi za elimu za juu China nzima.

Baada ya Maswali na Majibu kulikuwa na muda wa Ugawaji wa Vyeti- ambapo kulikuwa na ugawaji wa vyeti kwa Viongozi wa Kamati Tendaji ya TASAFIC 2017/2018 kuwashukuru kwa kazi nzuri waliyofanya; walitajwa kwa heshima na shukrani za kipekee kutoka kwa uongozi wa sasa wa Shrikisho na viongozi hao ni Hussein Mtoro (Aliyekuwa Mwenyekiti). Hamenya Mpemba (Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti), Remidius Mwema (Aliyekuwa Katibu Mkuu), Jospeh Cyrilli (Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu), na Rogers Paris (Aliyekuwa Muweka Hazina); Vyeti vyao hivi viliwasilishwa na kupokelewa na Rogers Paris ambaye bado yupo hapa China Kimasomo na ni kiongozi kwenye Jumuiya yake ya Tianjin.

Vyeti vya uwakilishi vilitolewa kwa Jumuiya mbalimbali, Picha za Makundi Mbalimbali, na kuhitimisha Mkutano kiujumla kulifuat baada ya hayo yote.

Kwa maazimio yaliyofanyika katika Mkutano huo ilipendekezwa kwamba Mwakani Mkutano Mkuu wa Watanzania wanaosoma China ufanyike Mjini NANJING.

 

WechatIMG782.jpeg

 

WechatIMG539.jpeg

 

 

JUMUIYA ZILIZOSHIRIKI KATIKA MKUTANO MKUU WA SHIRIKISHO LA JUMUIYA ZA WATANZANIA WANAOSOMA CHINA

 • BEIJING; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma BEIJING Iliwakilishwa na Viongozi Bi. Selwa Ali Sheha na Suleiman Mwenda.
 • DALIAN; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma DALIAN Iliwakilishwa na Viongozi Dr. Emmanuel S. Kinayi, Dr George Kanani na Dr Julieth Kajugusi.
 • JILIN; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma JILIN Iliwakilishwa na Viongozi Denis Mukama, Nangware Kajia Msofe, Seria Masole Shonyela.
 • JINZHOU; Watanzania wanaosoma JINZHOU waliwakilishwa kwa ujumla wao na Nicodemus Tesha, Massoud Mtore, Lidya Sameji, Kekiliya Kahinga, Sylvia Alice, Eric Kazoka, Emanuel Mabula, Victoria Mumangi, Emanuel Mallya, Benard Bwire, Vannesa Hans, Claudia Charles, Gwamaka Tumaini, Esther Dyson, Sameer Mohammed
 • HARBIN; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma HARBIN Iliwakilishwa na Kiongozi Bi. Victoria Mwanziva
 • HENAN; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma HENAN Iliwakilishwa na Viongozi Ibrahim R. Nyanza, Elizabeth Ndallo, Heri Issa Gombera
 • NANJING; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma NANJING Iliwakilishwa na Kiongozi Benson Mugaka
 • TIANJIN; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma TIANJIN Iliwakilishwa na Viongozi Eng. Nicas Bernard na Rogers Paris
 • WUHAN; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma WUHAN Iliwakilishwa na Viongozi Jaffar Mohammed na Rashid Mohammed Rashid
 • FUSHUN; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma FUSHUN Iliwakilishwa na takribani wajumbe 50 ambao waliongozwa na viongozi wao wa jumuiya yao; Albert Kent, Fadhili Nyamwinuka, Georgina Mgoyela, Thomas Mwabobo, Aisha Msantu, Halima Mussa na Martin Mwamukonda; walikuwepo pia Viongozi watsaafu wa Jumuiya ya Fushun kama Francis Magira na Stephen Beda ambao walishiriki moja kwa moja kwenye kamati wakisaidiana na viongozi wa sasa katika usimamizi kwani Fushun na Shenyang ni jumuiya ambazo zinakaribiana hivyo ushiriki wao ulikuwa mkubwa sana.
 • SHENYANG; Jumuiya ya Watanzania wanaosoma SHENYANG ambao ndio walikuwa wenyeji walikuwa na uwakilishi mkubwa wa wanajumuiya wao wakiongozwa na Viongozi wa Jumuiya zao; Racheal Kaali, Berrington Shayo, Lena Msuya, Warren Wilbert, Erick Paul, Lisa Rwebangila wakiwa na viongozi wengine wawakilishi wa vyuo vyao Shenyang, pamoja na wanakamati wa maandalizi wote kiujumla.

WechatIMG541.jpeg

 

WechatIMG790.jpeg

 

 

RIPOTI HII IMEANDALIWA NA

VICTORIA MWANZIVA

(Makamu Mwenyekiti Shirikisho la Jumuiya za Watanzania wanaosoma China- TASAFIC)

Pamoja na

STEPHEN BEDA

(Muwakilishi kutoka Jumuiya ya Watanzania wanaosoma Fushun- TSA LSU)

 

 

TAARIFA YA MKUTANO MAALUMU WA WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA NA WATANZANIA CHINA

WechatIMG324Mkutano Maalumu wa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ulifanyika Ubalozi wa Tanzania Beijing tarehe Septemba 2, 2018- ambapo alitumia nafasi hiyo kukutana na Watanzania Wanaofanya Biashara, Wanaofanya Kazi, Wanaosoma na Wanaoishi China.

Mheshimiwa Waziri Mkuu aliambatana na Viongozi wengine ambao walikuwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga; Mhe. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mhe. Rashid Ali Juma, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Viongozi wengine Waandamizi.

Mheshimiwa Waziri Mkuu amekuja China kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) unaofanyika Beijing, China. Ila akaona ni vema na sahihi akitupa nafasi Watanzania tuliopo China kwa shughuli mbalimbali, uwanja wa kutusikiliza na pia kusikia ujumbe kutoka kwake.

Kwa upande wa Shirikisho la Jumuiya za Watanzania Wanaosoma China (TASAFIC), Tuliwakilishwa vema na Mwenyekiti wetu ndugu Denis Mukama aliyewasilisha hotuba mbele ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na wageni wote waliokuwepo kwa niaba ya Watanzania Wanaosoma China.

Hotuba yake iligusa utambulisho wa Shirikisho letu la TASAFIC, pamoja na changamoto mbalimbali na maono tuliyoyawasilisha kupitia utaratibu ulioratibiwa na Katibu wa TASAFIC hapo awali.

Ushiriki wa Jumuiya za Tasafic Ulikuwa mzuri wa kuridhisha ambapo- TASAFIC Kamati Tendaji iliwakilishwa na Mwenyekiti Ndugu Denis Mukama, Makamu Mwenyekiti Bi Victoria Mwanziva, Muweka Hazina Bi Lucynancy John.

 

JUMUIYA MBALIMBALI ZILIWAKILISHWA KAMA IFUATAVYO:

Jumuiya ya Beijing inyayoongozwa na Ndugu Kulwa Gamba (Mwenyekiti Beijing).

Jumuiya ya Beijing ilikuwa mwenyeji wetu mkuu wa Shughuli hii, na walikuwa na uwakilishi mzuri kwenye shughuli hii.

Jumuiya ya Harbin iliwakilishwa na Bi Victoria Mwanziva (Makamu Mwenyekiti Harbin, Makamu Mwenyekiti TASAFIC)

Jumuiya ya Henan iliwakilishwa na Bi Phelister Wegesa (Mwenyekiti Henan)

Jumuiuya ya Jilin iliwakilishwa na Mwenyekiti Denis Mukama (Mwenyekiti Jilin, Mwenyekiti TASAFIC)

Jumuiua ya Jinhua iliwakilishwa na Lucynancy John (Muweka Hazina Jinhua, Muweka Hazina TASAFIC)

Jumuiya ya Qingdao iliwakilishwa na  Yazid Iddi (Mwenyekiti Qingdao)

Jumuiya ya Shanghai iliwakilishwa na Bi. Angel Richard Kessy, Dafina, Ndugu Charles

Jumuiya ya Shenyang Iliwakilishwa na Ndugu Berrington (Makamu Mwenyekiti Shenyang)

Na Jumuiya ya Tianjin iliwakilishwa na viongozi wao ambao ni Martin Itangaja (Katibu  wa kamati ya jamii na michezo), Joyce Ndauka- (Kaimu katibu). Hija Athman (Mwenyekiti kamati ya nidhamu, Sheria na Katiba). Beatrice Mushi- (Katibu kamati ya fedha na Mikopo) Pamoja na wanachama Castro Mwankefu- (Mwanachama), Bahati Gasper Mteti- (Mwanachama)

UJUMBE KUTOKA KWA WAZIRI MKUU:

Mheshimiwa Waziri Mkuu aligusia masuala mengi sana kwenye hotuba yake kwenye mkutano maalumu uliofanyika kati yake na Watanzania waliopo China- Masuala Makuu muhimu yanayotugusa ni kama yafuatayo-

Watanzania tulipo China tudumishe Umoja, kwani Umoja ndio msingi wa mafanikio- amepongeza uwepo wa TASAFIC na amesisitiza sana tuudumishe umoja huu kadri ya uwezo wetu.

Matumizi ya Elimu yetu kwa Manufaa ya Kuinua Tanzania:

Amesisitiza Watanzania tuliopo China- tufanye tafiti mbalimbali za kitaaluma na kuhakikisha kuwa taaluma hizi tuzisomeazo zitakuja kuinua taifa letu la Tanzania.

Juhudi katika masomo- Mheshimiwa Waziri Mkuu amesisitza sana tujitahidi kujituma katika masomo yetu ili tuweze kumaliza tukiwa na ujuzi mzuri kutoka huku China

Mheshimiwa Kassim Majaliwa Kassim ang’oa mzizi wa Mawakala wasio waaminifu kwa kuamuru papo hapo mkutanoni baada ya kusikia kilio cha wanafunzi wengi kuhusiana na masuala ya Mawakala- ameamuru kuwa Mawakala wote wanapaswa kujisajili Wizara ya Elimu waweze kutambulika- na waweze kufanya kazi kwa mipaka ya Wizara ya Elimu. Gharama zao hazipaswi kwenda kuumiza Watanzania katika huduma wazitoazo.

Lakini Watanzania wote wanaopata nafasi za kimasomo kupitia Mawakala wanapaswa kufikishiwa taarifa zao Ubalozini na mawakala hao ili kila Mtanzania anayeingia nchi husika atambulike Ubalozini.

Masuala ya vyeti vya wahitimu kutoka China katika Taaluma mbalimbali;

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Wahitimu wanaohitimu China- wanapaswa kuhakikisha taarifa za kozi zao zipo sahihi ili vyeti vinaporudi Tanzania na kuhakikiwa na TCU ziwe na uhakika haswa kwenye suala la Specialization za kozi zao husika.

Aidha amemuagiza Mheshimiwa Waziri wa Elimu kufuatilia kwa Karibu suala hili.

Aidha Mheshimiwa Waziri Mkuu aligusia kuhusiana na suala la kuendelea kushikamana na Ubalozi, katika hatua zetu zote. Amempongeza sana Mheshimiwa Balozi Kairuki kwa kazi kubwa anayoifanya hapa China.

Salaam nyingi zimewasilishwa kwetu sote na Viongozi waandamizi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliozungumza katika hafla hiyo akiwemo Waziri wa Mambo Nje Mheshimiwa Balozi Augustine Mahiga aliyeainisha historia ya Ushirikiano baina ya China na Tanzania pamoja na umuhimu wa kuutunza umoja wetu huu.

Uongozi wa Shirikisho la Watanzania Wanaosoma China unashukuru sana Ubalozi wa Tanzania nchini China kuandaa hafla hii muhimu ambayo tulipewa fursa ya kushiriki, na kusikia mengi kutoka kwa Waziri Mkuu-

Aidha tunashukuru Uongozi wa Jumuiya ya Beijing Ukiongozwa na Mwenyekiti Ndugu Kulwa Gamba na Wana TZSUB wote kwa upendo wao na umoja wao haswa juu ya mapokezi mazuri ya Wanashirikisho kutoka majimbo mbalimbali waliofikia Beijing kwa ajili ya mkutano huu.

Aidha pia tunashukuru kwa umoja wetu Viongozi na wawakilishi waliojitolea kwa moyo mmoja kushiriki katika Shughuli hii muhimu- kuwakilisha Jumuiya zao na kushiriki kikamilifu na watanzania wenzao katika hafla hii muhimu ambayo ilituleta pamoja na kutupa nafasi ya kujumuika kwa pamoja na kubadilishana mawazo na kujadili masuala mbalimbali ya Ustawi ya Jumuiya zetu.

Umoja wetu ndio msingi wa maendeleo na ustawi wetu.

 

Victoria Mwanziva

Makamu Mwenyekiti Shirikisho la Jumuiya za Watanzania Wanaosoma China (TASAFIC)

Septemba 3, 2018

THE INTERNATIONAL STUDENT CONFERENCE ON ENVIRONMENT AND SUSTAINABILITY (ISCES) VICTORIA MWANZIVA

THE INTERNATIONAL STUDENT CONFERENCE ON ENVIRONMENT AND SUSTAINABILITY (ISCES)

 

WechatIMG96

The “2018 International Student Conference on Environment and Sustainability (ISCES 2018)” was an international conference co-hosted by Tongji University and the United Nations Environment Program (UN Environment), and organized by UN Environment-Tongji Institute of Environment for Sustainability (IESD).

I Victoria Charles Mwanziva from The United Republic of Tanzania; currently a Masters of Public Administration Student at the Harbin Institute of Technology, was one of the Youths who were selected to participate in this International forum which brought together participants from over 50 countries. It was an outmost privilege to have been one of the selected Youth participants to this Global Youth Forum. It was an honor to represent my country Tanzania as well as my University Harbin Institute of Technology; and to have fully participated in such a forum and win an award at the end of the forum for “Best Presentation”.

The “2018 International Student Conference on Environment and Sustainability (ISCES 2018)” (June 2-7 2018) Shanghai, China was launched on the World Environment Week this year. In response to the proposal to build a beautiful China by the Chinese government and the World Environment Day theme, the topic of ISCES 2018 was “Less plastic, better city life.” The themes were; 1) Education for Sustainable Development (ESD); 2) Food and Health; 3) Ecosystem and Climate Change; and 4) Green Development. The conference was beneficial in promoting awareness, capacity and networking amongst students, as future leaders, policy makers and activists and updating them of recent challenges and developments in the area of environment and sustainability.

Various high-level panel discussion on Education for Sustainable Development (ESD) and green development were arranged after the opening ceremony. There were three other side events which were held during the conference.

On June 5, The UN Environment-Tongji Institute of Environment for Sustainable Development (IESD), the organizer of this conference, Xinhua News Agency and Global Universities Partnership on Environment and Sustainability (GUPES) had jointly held a forum entitled “Towards the Future: Education for Sustainable Development (ESD) in Higher Education. Where I participated fully in this event and represented well;

On June 3 and 4, I along all of the participants had participated in field trips to demonstrate the development of Tongji’s sustainability-oriented university, Shanghai green urban development, ecological agricultural production and food safety.
On June 6, there was the CUE2018: Applied Energy Symposium and Forum on Urban Ecology and Energy Conservation: Low Carbon Cities and Urban Energy Systems and side events on young scholars’ SD projects, as well as competitions on poster, papers, presentations. I participated in this forum on Energy as it is one of my areas of interest and where my thesis paper will be focused on, participating in this forum had given me an understanding on how to well represent my ideas about the energy sector- and insights on Energy issues.

On June 7th, was the closing ceremony centering on “Less Plastic Pollution, Better City Life”, the International Student Conference on Environment and Sustainability 2018, co-hosted by the United Nations Environment Programme, Tongji University, Xinhua News Agency and Beijing Environment Foundation for Young Talents, concluded in Tongji University where around 300 youth students from 50 countries and regions jointly made the announcement of Global Youth Tongji Declaration.

The Declaration said that our stand as a global community to beat plastic pollution aligns with our core belief that the ecosystem cannot be isolated from humans. Now we should reflect our actions and lead at the fore front the charge against plastics and their toxic deleterious impacts on our environment, to keep marine organisms from danger and never to create worlds of plastics in any form or shape with a core in creating a harmonious relationship between nature and mankind. I was part of the team that drafted the declaration.

On the closing ceremony, Mr. Ananda Dias, Asia-Pacific Regional Coordinator for Early Warning and Assessment, UN Environment Regional Office for Asia and the Pacific,Prof. Li Fengting, Executive Deputy Dean of IESD, Deputy Dean of College of Environmental Science and Engineering, Tongji University, Ms. Qian Xin, Vice Chairperson of College University Council of Environmental Science and Engineering represented attendees to award such prizes as “Best Poster Prize” and “Best Presentaiton Prize” in order to encourage youth students to continue to pay attention to environment and sustainability and enjoy a green lifestyle.

These awards were presented to those who stood out in such activities as group discussions, reports and poster making, elected by students from groups of energy transition and climate change, eco-city, ecosystem and wildlife, and green lifestyle. I Victoria Mwanziva was one of the winners of the Best Presentation award, and it was an outmost honor to be able to represent my Country Tanzania and my University the Harbin Institute of Technology well.

During the six-day conference, we the participants took part in series of reports, universities students sustainable development project report, exhibitions, summit and on-site visits which were all very useful and advantageous to our learning.

I am grateful and it means a lot to me to have been able to represent my University and my country Tanzania in such an international forum and more importantly win an award. I urge youths to be proactive and fully participate in searching for such opportunities.

 

WANAWAKE NA MAENDELEO

“WANAWAKE NA MAENDELEO”

 IMG_4308

Siku ya wanawake Duniani- Inaaadhimishwa Kila ifikapo Tarehe 8 Mwezi wa Tatu Kimataifa; kuna umuhimu mkubwa wa kuutambua mchango wa wanawake katika nyanja Mbalimbali na kumuinua Mwanamke azidi kusimama na kuinuka kimaendeleo katika Jamii ulimwenguni kote.Lengo kuu la kuadhimisha siku hii adhimu ni kutathmini utekelezaji wa afua za kufikia usawa jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi, kijamii, kisiasa katika kufikia maendeleo jumuishi. Maadhimisho haya, pia yanatoa fursa ya kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na jamii, serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na wadau wa maendeleo katika kumwinua mwanamke.

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu kupitia kaulimbiu ya ‘Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini’, amewataka wanawake kutambua kuwa serikali imekuwa ikiwahudumia, kuwathamini, kuwawezesha na kuwasimamia vyema ili kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwepo katika jamii. Makamu wa Rais amebainisha mambo hayo saba kuwa ni:

 

 • Kuwepo kwa Sera ya Kuendeleza Wanawake,

 

 • Sheria za Ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi,

 

 • Sera ya Elimu Bure inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo imetoa fursa kwa watoto wengi wa kike kuandikishwa shuleni.

 

 • Kuboreshwa kwa huduma za kijamii, kama vile kujengwa zahanati na vituo vya afya na usambazaji wa maji, vimempunguzia mwanamke usumbufu na hivyo kumpa muda wa kutosha kufanya shughuli za maendeleo.

 

 • usambazaji umeme vijijini, kwa kiasi kikubwa umesaidia wanawake wengi, kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato.

 

 • Uwezeshaji wa wanawake kwa kuwapatia asilimia 5 ya mapato ya halmashauri na asilimia 30 ya zabuni za halmashauri, kumewawezesha wengi kufanya biashara na hatimaye kuwa na uhakika wa kipato.

 

 • Urasimishaji wa vikoba pamoja na kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuweza kunufaika na mafao na mikopo itolewayo na taasisi hizo.

 

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania; iliridhia Itifaki ya Maendeleo na Jinsia ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika; ambayo imesisitiza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi kitaifa katika kila taifa lililoridhia Itifaki hiyo ya Maendeleo. Tanzania imefanikiwa kufikia asilimia 37 ya wanawake Bungeni, asilimia 41 wanawake majaji na asilimia 30 wanawake madiwani. Kutokana na jitihada hizo wanawake wanaendelea kuaminika na kuchukua nafasi za juu za uongozi na maamuzi ikiwemo nafasi ya Makamu wa Rais na Naibu Spika.

 

Wanawake wameendelea kuimarika katika Nyanja mbalimbali, katika Sekta mablimbali muhimu kama vile- Sekta ya Afya, Elimu, Kiuchumi, Huduma za Kijamii ambapo tunazidi kuona siku hadi siku wanawake wanavyojituma na kusonga mbele. Kuna baadhi ya Sekta kama Madini, Uhandisi, Uchumi- mwanamke anazidi kusonga mbele kwa kuchukua nafasi za uzalishaji, kushiriki kikamilfu katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini Tanzania.

 

Tukiwa kama Wanawake wa Kitanzania tunaosoma China, tunazidi kuwahamasisha na kuwaambia wenzetu wote- wanaosoma na ambao wapo katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo kuwa; inawezekana- tuna uwezo, tuna nguvu na tunatakiwa tusonge mbele daima kwasababu tuna kila sababu ya kuwa mstari wa mbele kupambania maendeleo ya Nchi yetu ya Tanzania.

 

Victoria Mwanziva

Harbin Institute of Technology

Jumuiya ya Watanzania Wanaosoma Harbin (TASAHA)

2018 MWAKA WA KUZIISHI TUNU ZA TAIFA MAKALA YA VICTORIA MWANZIVA

2018 uwe Mwaka wa Baraka na Mafanikio kwetu sote; Tukaongeze Juhudi katika kila tufanyalo lenye lengo la Kuinua Wenzetu; Kuinua Jamii Zetu; Kuinua Nchi na Bara letu. Ifike wakati Vijana tutambue nafasi tulizonazo katika kupambania maendeleo ya Nchi Yetu katika Nyaja; Kijamii; Kiuchumi; Sayansi na Teknolojia; Utabibu; Ubunifu; Sanaa; na Taaluma zote
Tuziishi tunu zetu za Taifa la Tanzania- Utu; Uzalendo; Uadilifu; Umoja; Uwazi; Uwajibikaji; na Tuendeee kukuza na Kuinua Lugha yetu ya Taifa. Vijana Ndio chachu ya kuendeleza miiko na maadili ya Nchi Yetu; Vijana Ndio chachu ya Maendeleo na tunatakiwa kujitambua na kutambua Nafasi Yetu Katika kuinua Nchi yetu kila mmoja Katika Nafasi aliyonayo. Sisi Ndio tutaotengeneza Tanzania tunayoitaka; Juhudi ya Kila mmoja inahitajika Katika Kuhakikisha hili linafanikiwa.
Utu Ni nguzo kuu- Tutangulize Utu Katika matendo yetu yote- tuwe waungwana; wapenda haki; wenye kauli njema; wenye hekima.
Uzalendo ni nguzo Muhimu kwani tukitambua Kuwa Juhudi zetu kila mmoja zikijumuishwa tutaipata Tanzania tunayoihitaji. Tuipende na Tuitangaze nchi Yetu ya Tanzania Kila mmoja wetu aibebe Nchi Yetu moyoni na Katika Matendo Yake.
Uadilifu wetu ndio utakaoonesha mafanikio; Katika Nyanja zote
Umoja kwangu nawaza kusema ndio Tunu ya Muhimu haswa kwetu Vijana kwani tunatambua usemi usemao “Umoja Ni Nguvu; Utengano Ni Udhaifu” Umoja wetu ndio utakaotupa yale matunda na mafanikio tunayotamani kuyaona
Uwazi Ni muhimu; nahisi Kuwa hii Kila mtu anaweza kutafsiri ajuavyo Yeye Ila Mimi nimeitafsiri Kwa Dhana ya Ushirikiano na Kuinuana baina yetu- Tuwekane wazi Juu ya Fursa mbalimbali; tuinuane na tushirikiane
Uwajibikiaji Ni nguzo ya Muhimu kwetu Vijana Kwa Mantiki ya Kuhakikisha Tunawajibika Kila mmoja Katika Nafasi yake. Kila mtu afanye Kazi kadri ya nafasi aliyonayo- popote alipo atambue Kuwa Yeye Ni Chachu ya Maendeleo na mafanikio. Tusikae tukinyooshea mtu na kusema Hii Ni Kazi Yake bali tujitathmini na tuangalie Nafasi zetu Sisi Ni zipi; na tujitathmini kipi tunachoweza Kufanya Kuhakikisha tunatengeneza mazingira bora Zaidi ya Nchi yetu kiujumla.
Kila la Kheri kwetu sote; Katika Kuwajibika; Kujituma; Kuinuana na Kufikia Makengo yetu Katika Mwaka 2018.

IMG_5020Victoria Mwanziva